Cari Blog Ini

Tuesday, April 21, 2026

KUHUSU AWLF

💬 : 0 comment

 

AL-WAQF LILLAAHI FOUNDATION

*JINA LA SHIRIKA:*
AL-WAQF LILLAAHI FOUNDATION

ni shirika lisilo la kiserikali linalojitolea kuhudumia jamii kwa misingi ya kujitolea, huruma, na uadilifu. Likiongozwa na kaulimbiu IHSAN KATIKA JAMII

*MALENGO YA SHIRIKA (OBJECTIVES)*

1. Lengo Kuu (Main Objective)

Kuinua hali ya maisha ya jamii na kupunguza umaskini kupitia utoaji wa huduma bora za kijamii, kukuza elimu, na kuimarisha miradi endelevu ya kiuchumi na kiroho kwa misingi ya kusaidiana na kujitolea.

2. Malengo Mahususi (Specific Objectives)

a) Sekta ya Elimu na Maadili:

* Kukuza na kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto na vijana kutoka mazingira magumu kupitia misaada ya ada, vifaa, na sare za shule.

* Kujenga na kusimamia miundombinu ya elimu (kama Madrasa na shule) ili kuimarisha maarifa na maadili mema kwa vijana dhidi ya vitendo hatarishi kama dawa ya kulevya na uhalifu.

b) Ustawi wa Jamii na Misaada ya Kibinadamu:

* Kutoa misaada ya dharura ya kibinadamu (chakula, mavazi, na malazi) kwa wahitaji, yatima, wajane, wazee, na watu wenye ulemavu.

* Kuratibu na kutoa misaada ya haraka wakati wa majanga ya asili kama njaa, mafuriko, au moto.

c) Afya na Mazingira:

* Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu lishe, usafi, na kinga dhidi ya magonjwa, pamoja na kusaidia wagonjwa wasiojiweza kupata huduma za matibabu.

*Kushirikiana na serikali na wadau wa afya katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwenye jamii.

d) Uwezeshaji wa Kiuchumi:

* Kuanzisha na kusaidia miradi midogo midogo ya kujiongezea kipato kwa vikundi vya wanawake na vijana kupitia mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha.

e) Miradi Endelevu ya Waqf (Sadaka Endelevu):

* Kuhamasisha na kusimamia uwekezaji katika miradi ya Waqf (kama majengo au mashamba) ambayo mapato yake yatatumika kuendesha shughuli za kijamii na kuhudumia taasisi za kidini kwa muda mrefu.

f) Ushirikiano na Mitandao:

* Kujenga ushirikiano na serikali, taasisi binafsi, na mashirika ya kimataifa ili kuleta maendeleo jumuishi na endelevu kwa jamii.


No comments:

Post a Comment